Thursday, October 10, 2019




RAMADHANNswanzurimo, Kocha Mkuu wa Singida United, amepewa jukumu jipya la kupata ushindi kwenye mechi zake zote za mwanzo ili kuiokoa timu isishuke daraja.

Nswazurimo amebeba mikoba ya Felix Minziro aliyekuwa anainoa timu ya Mbeya City kabla ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wamempa majukumu mazito kocha huyo ili arejeshe ubora wa timu ya Singida United.

“Tunatambua kwamba kwa sasa timu inapita kwenye mapito ambayo yalikuwa yanasababishwa na ugeni wa timu kwa kuwa tumempata kocha mpya tuna imani kutakuwa na mabadiliko makubwa.

“Moja ya kazi ambayo tumempa ni kuona kwamba anaibadilisha timu na kuleta matokeo chanya kwenye timu hasa kwenye mechi ambazo tutacheza kwani mashabiki wanahitaji kupata matokeo,” amesema Katemana.

0 comments:

Post a Comment