Thursday, October 10, 2019

  
BEKI mkongwe na kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani ameongeza idadi ya majeruhi kwenye kikosi hicho baada ya kupata maumivu ya misuli huku kiungo fundi Mkongomani, Papy Tshishimbi akirejea mzigoni.


Loading...

Yondani alitolewa kwenye kipindi cha pili wakati timu hiyo ilipocheza na Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa



Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na matokeo kumalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0, wikiendi iliyopita.

Mara baada ya beki huyo kupata majeraha na kutolewa nje alliingia Mrundi, Mustafa Suleyman kuchukua nafasi yake.



Akizungumzia hilo Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavo alisema: “Yondani anaendelea na matibabu baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wetu wa ligi na Coastal Union na kusababisha ashindwe kuendelea na mchezo huo.



“Hivyo bado anaendelea na matibabu wakati wowote atarejea uwanjani, Tshishimbi yeye tayari amepona na leo (jana) asubuhi ameanza mazoezi ya pamoja na wenzake.”



Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ni Lamine Moro, Raphael Daudi, Patrick Sibomana, Mohammed Issa ‘Banka’, Paul Godfrey na Sadney Urikhob

0 comments:

Post a Comment