Uongozi
wa klabu ya Mtibwa Sugar hadi sasa upo njia panda kufuatia kufungiwa
kwa viwanja vyake vyote ilivyokuwa inachezea mechi za nyumbani kunako
Ligi Kuu Bara.
Ikiwa
ni wiki kadhaa tangu kufungiwa Uwanja wa Manungu, Mtibwa ilipangiwa
kutumia uwanja wa Jamhuri ambao nao wiki hii umetangazwa kufungiwa na
Bodi ya Ligi.
Saleh
Jembe ilizungumza na Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, ambaye
aliibuka na kusema kuwa hadi sasa wapo njia panda kuwa watatumia uwanja
gani.
"Kiukweli hatujajua maana Manungu ilifungiwa na sasa Jamhuri nayo pia imefungiwa.
"Tunachoomba
sisi TFF na Bodi ya Ligi waturuhusu tutumia huu wa Manungu sababu
tunaingia kwenye gharama kubwa sana kupeleka timu Jamhuri, inakuwa kama
tunaenda ugenini.
0 comments:
Post a Comment