Thursday, October 10, 2019



Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi, anayekipiga katika Klabu ya Al Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, amefikisha dakika 205 bila ya kufunga bao, huku akiambulia kadi ya njano.

Mpaka sasa Okwi amecheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Misri, huku mechi mbili dhidi ya Zamalek na El Gouna akicheza kwa dakika zote tisini, huku dhidi ya Al Masry akiingia dakika ya 65.

Mshambuliaji huyo ambaye ana rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 207/18, msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao 15.

Kutokana na ukame huo wa mabao akiwa nchini Misri, jambo hilo limezua sintofahamu ya kwamba huenda mchezaji huyo akawa ameshindwa kung’ara katika ligi hiyo.

0 comments:

Post a Comment