Mwanariadha
wa Kenya bingwa wa Olimpiki katika mashindano ya marathon, Eliud
Kipchoge ametunukiwa tuzo ya kitaifa ya rais uhuru Kenyatta.
Rais Kenyata ambaye anaongoza sherehe za Mashujaa Day mjini Mombasa pwani ya Kenya amemsifu mwanariadha huyo kwa kuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili mjini Vienna.
“tuzo ya mashujaa wote ,waliopita, wasasa na wajao, unamuendea Eliud Kipchoge,”Uhuru, alisema mwisho wa hotuba yake huku tangazo hilo likishangiliwa kwa vifijo.
“Eliud Kipchoge anasalia kuwa shujaa mashuhuri katika nchii hii. Ushindi wake wa hivi karibuni unatukiumbusha kuwa mtu anaweza kufikia malengo yake binafsi na yale ya taifa kwa ujumla,” rais alisema
Baada ya hapo alimualika Kipchoge kujumuika naye jukwani, kumsalimia na kisha kumvisha taji maalum kwa ajili ya utambulisho wa tuzo hiyo.
Rais pia alimtambua mwanariadha Brigid Kosgei ambaye hivi karibu alivunja rekodi ya wanawake ya mbio za marathon mjini Chicago.
Kipchoge, hivi karibuni alitangazwa kuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili.
Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindani la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria.
Ushindi huo haukutambuliwa kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kusukuma kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.
Katika hotuba yake kwa taifa rais Kenyatta alitoa wito kwa Wakenya kuiga mfano wa mwanariadha huyo ili kufikia malengo ya kibinafsi na ya kitaifa.
0 comments:
Post a Comment