Monday, October 14, 2019



Baada ya timu ya Italia kufuzu kucheza fainali za Euro 2020 ikiwa na michezo mitatu mkononi baada ya kupata ushindi katika michezo yake yote saba waliocheza na kufikisha jumla ya point 21 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya Kundi lao J, michezo ya Euro kufuzu inaendelea tena Jumatatu ya October 14 na 15.
Ureno ikiwa na nahodha wao Cristiano Ronaldo October 14 italazimika kwenda hadi nchini Ukraine kucheza mchzo dhidi ya taifa hilo wakati ambao Ronaldo anaingia akiwa na kumbukumbu ya kuweka rekodi ya kufunga jumla ya magoli 699 aliyofunga wiki iliyopita, mchezo huo wa Kundi B utakuwa ni mgumu kutokana Ukraine wao kujiweka pazuri kwa kuwa na point 16 kileleni na Ureno wakiwa wapili kwa point 11 ila Ukraine ameizidi mchezo Ureno, game hii itaonekana Star Times
Ufaransa na Uturuki ambao kila mmoja anahitaji point 4 ili kufuzu kutokana na wote kufanana point kila mmoja akiwa na 18 ila wametofautiana magoli ya kufunga na kufungwa, wao watacheza pia October 14 Ufaransa akiwa nyumbani kuwakaribisha, wakati England watacheza na Bulgaria michezo mingine ya kuvutia itachezwa October 15 Sweden dhidi ya Hispania na Switzerland dhidi ya Ireland ikichezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki, itaonesha kwenye ST World Football na Sports Premium.
Ratiba ndio hii game zote zitachezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki.

0 comments:

Post a Comment