Patrick
Aussems, kocha mkuu wa Simba ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji
ametangaza hali ya hatari kwa wapinzani wa Simba ambao atakutana nao
kwenye mchezo wao unaofuata wa ligi.
Aussems
aliondoka nchini Tanzania Jumatatu ya wiki hii kimyakimya na kurejea
nyumbani kwao Ubelgiji kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na sababu
zake binafsi na aliahidi kurejea jana akiwa na hasira za kupata pointi
tatu za Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nane na ina pointi 15. Kupitia
ukurasa wake wa Instagram Aussems amesema:”
"Niliondoka
kwa sababu zangu binafsi mwenyewe kwa siku mbili nitarejea kesho
(jana), kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting
nazihitaji pointi tatu.
”
Championi Jumatano, lilizungumza na Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu
ambaye alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala la kocha kwa kuwa bosi wao
ameshazungumza.
“Bosi
amesema kuwa hajui alipo kocha sasa mimi nitazungumza nini hapo, zaidi
ya kufuata kile ambacho amesema CEO? (Mkurugenzi Mtendaji) basi kwa kuwa
mwajiri hajui alipo mfanyakazi wake hakuna nitakachoweza kuzungumza,”
alisema Rweyemamu.
Simba
inatarajiwa kushuka Uwanja wa Uhuru Novemba 24 kumenyana na Ruvu
Shooting mchezo wao wa 10 kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza baada ya
kucheza mechi 9 na imejikusanyia pointi 22, imepoteza mchezo mmoja mbele
ya Mwadui FC na imeshinda mechi saba na sare moja dhidi ya Prisons

0 comments:
Post a Comment