Tuesday, December 24, 2019


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ametokea benchi nusu saa ya mwisho, timu yake, KRC Genk ikichapwa 2-0 na wenyeji, Anderlecht katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Lotto Park mjin Brussels.
Samatta ambaye leo anafikisha umri wa miaka 27, aliingia kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mnigeria, Ebere Paul Onuachu dakika ya 62, wakati mabao yaliyowazamisha Genk jana yalifungwa na kiungo Mholanzi mwenye umri wa miaka 22, Michel Vlap dakika ya 54 na 61.
Na kwa matokeo hayo, mabingwa watetezi wa Ubelgij, Genk wanaoshika nafasi ya nane kwa pointi zao 28, sasa wanaizidi Anderlecht pointi mbili tu baada ya wote kucheza mechi 19.
Jana Samatta amecheza mechi ya 182 katika katika mashindano yote akiwa amefunga mabao 71 tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 141 akiwa amefunga mabao 54, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi 10, amefunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi sita, mabao matatu.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vandevoordt, Maehle, Dewaest, Lucumi, Neto/Odey dk82, Berge, Hrosovsky, Ito, Bongonda/Hagi dk62, Paintsil na Onuachu/Samatta dk62.

0 comments:

Post a Comment