Victoria Conteh: Kocha mwanamke anayeweka historia Sierra Leone kwa kufunza katika ligi kuu Victoria Conteh ameteuliwa kuwa mkufunzi wa kwanza mwanamke kuifunza klabu ya wanaume katika ligi ya Sierra Leone kwa sababu amefuzu kufanya hivyo, kulingana na mmiliki wa klabu hiyo. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 ni mwanamke wa pili kusimamia klabu ya ligi ya daraja la juu ya wanaume barani Afrika baada ya mwanamke mwengine wa Ethiopia kocha Meseret Manni anayeifunza klabu ya wanaume ya Dire Dawa mwaka 2015. Klabu ya East End Tigers iliokuwa ikijulikana kama Gem Stars ya Tongo wamemuajiri mchezaji huyo wa zamani kwa kipindi cha miaka miwili. ''Tuliamua kumuajiri kwasababu anafuzu na hicho ndio kilichokuwa kigezo'', alisema mmiliki Victor Lewis akizungumza na BBC. ''Sio kuchagua mwanamume ama mwanamke kigezo hapa ni kufuzu kufanya kazi hiyo. Helena Costa kufunza wanaume Ana kandarasi ya miaka miwili na tumempatia lengo letu la kumaliza katika timu nne bora na tuna matumaini makubwa kwamba atafanikiwa. Conteh ndio kocha mwanamke wa pekee aliyepewa leseni na Caf katika taifa hilo na awali alikuwa akiifunza timu ya taifa ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 mbali na timu ya wanawake ya polisi wa Sierra leone. Lakini sio mgeni kwa mchezo wa wanaume , baada ya kuisimamia kwa muda klabu ya wanaume iliopo katika ligi ya pili Delta Strikers. ''Nafurahia na najivunia kuhusu ajira hii na nimeichukua na mikono miwili . Hii ni zawadi yangu ya Krisimasi kwasababu nilikuwa nikiitarajia''. ''Najua sio rahisi kwa mwanamke kuhudumu kama kocha katika ligi kuu ya Sierra leone lakini nitakabiliana na presha iliopo na nitajitahidi kufanya vyema''.
0 comments:
Post a Comment