Kuelekea
pambano la watani wa jadi Simba na Yanga linalotarajiwa kufanyika
Jumamosi wiki hii, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
limewaonya mashabiki wa timu hizo kwa kuwataka kuwa wastaarabu wakati
wote wa mchezo huo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro
Mambosasa, alisema wamejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi katika
mchezo huo, akiwataka mashabiki wote watakaofika kutazama mchezo huyo
kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Alisema
pamoja na mapenzi yao kwa timu hizo, mashabiki hao wanatakiwa
kushabikia mchezo huo kwa ustaraabu bila kurushiana chupa na kuharibu
miundombinu ya uwanja na mambo mengine jambo litakaoufanya mchezo huo
kumalizika kwa amani.
“Hatutasita
kuwachukulia hatua kali watu wote watakaofanya mambo yasiyo ya
kistaarabu siku ya mchezo huo, tutakuwa tumejipanga na kujiimarisha
katika maeneo yote ya uwanja ili kuhakikisha mchezo unamalizika bila
kuwapo na vurugu kutoka kwa mashabiki,” alisema Mambosasa.
0 comments:
Post a Comment