Baada
ya kufunga bao lake la kwanza katika Klabu ya Yanga, ambalo liliipa
timu hiyo ushindi mbele ya Biashara United, mshambuliaji mpya Tariq
Seif, amesema kuwa sasa atafunga kwenye kila mchezo atakaopata nafasi ya
kucheza.
Tariq
aliibuka shujaa baada ya kufunga bao dakika za mwisho lililoipa ushindi
Yanga dhidi ya Biashara kwenye mchezo uliochezwa Jumatatu ya wiki hii
katika Uwanja wa Taifa, Dar na kuisaidia timu hiyo kuvuna alama zote
tatu na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 24.
Tariq
alisema kuwa kitendo cha kufunga bao la kwanza kwenye mchezo dhidi ya
Biashara United, kimempa moyo zaidi wa kufanya makubwa kwenye klabu hiyo
ambapo kwa sasa atajituma zaidi ili awe anafunga kwenye kila mchezo
atakaopata nafasi ya kucheza.
“Kiukweli
bao ambalo nilifunga jana (juzi) limeniongezea nguvu sana ya kupambana,
unajua nilikuwa nimekaa nje kwa muda mrefu bila kucheza, kwa hiyo
kitendo cha kurudi uwanjani na kufunga kimenipa moyo na sasa nitaongeza
juhudi zaidi ili niweze kufunga kwenye kila mchezo,” alisema Tariq.
Kauli
ya Tariq inakuwa kama inaibua hofu Simba kutokana na kuwa atakuwa
anakutana dhidi yao Januari 4, mechi itakayofanyika katika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Tariq
amejiunga na Yanga wakati huu wa dirisha dogo la usajili akitokea
katika Klabu ya Dekernes inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri,
lakini pia alishawahi kupita katika klabu ya Stand United na Biashara
United zote kutoka Tanzania.
0 comments:
Post a Comment