Thursday, January 30, 2020



BODI ya ligi (TPLB) imetoa onyo kwa waamuzi watatu wa mpira wa miguu kutokana na kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu katika mechi walizo chezesha.

Maamuzi hayo yametangazwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwenyela mbele ya vyombo vya habari katika makao makuu ya ofisi za Shirikisho la  soka Tanzania (TFF) zilizopo Karume jijini Dar es Salaam.

Waamuzi hao waliopewa onyo kali ni mwamuzi Floretina Zabron aliyechezesha mpambano wa ligi kuu namba 17 kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga mchezo huo uliopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya, mwamuzi huyu amepewa onyo hilo kutokana na kushindwa kutafsiri sheria licha ya uwanja kujaa maji kutokana na mvua kubwa kunyesha katika jiji la Mbeya.

Waamuzi wengine ni Jonesi Rukya na msaidizi wake Soud Lilla nao wamepewa onyo kali baada ya kushindwa kuona baadhi ya matukio yaliyojitokeza katika mchezo wa ligi kuu wa Simba na Yanga uliopigwa Januari 4 2020 katika dimba la Taifa

0 comments:

Post a Comment