Mwenyekiti
wa Klabu ta TP Mazembe ya DR Congo, Moses Katumbi, ameibuka na kumfunda
Bilionea mwenzake, Mohamed Dewji ‘Mo’ ili ajue miko ya kuwa mwekezaji
na mshabiki. Imeelezwa.
Dewji
licha ya kuwa ndiye mwekezaji Mkuu katika klabu ya Simba, lakini
amekuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo kiasi cha kukosa raha pale
inapotokea kikosi chake kupoteza mchezo.
Ni
juzi katika mashindano ya Mapinduzi CUP wakati timu hiyo ilipopoteza
mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar kwa
kuchapwa bao 1-0, alifikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti
wa Bodi lakini baadaye alibatilisha uamuzi wake.
Taarifa
imeeleza Katumbi alisema, anatambua machungu ambayo ameyapata baada ya
Simba kufungwa na MTibwa Sugar katika Kombe la Mapinduzi, lakini ndio
mpira ulivyo asitarajie matokeo chanya kila siku.
Alisema,
anatambua mchango wake mkubwa ndani ya Klabu hiyo, ambayo kwa sasa
inajulikana Afrika nzima, lakini amekuwa akichanganya kazi ya soka
pamoja na ushabiki mambo ambayo hayaendi sambamba.
“
Mo anapaswa kupata mafunzo kutoka kwa wawekezaji wakongwe kama sisi, ni
mara nyingi timu inaharibu lakini unalia na kufuta machozi kimya kimya,
haupaswi kuweka hisia zako kwa mashabiki kwa kuwa wao pia wanakutegemea
wewe”
Ushauri
wangu kwake, Simba ni Klabu kubwa sana Afrika, asikate tamaa, azidi
kupambana, kwani mafanikio ya Simba ni ya taifa la Tanzania sio
mashabiki peke yao,”alisema Katumbi.
Kwa
upande wa aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyoo, Crecentius
Magori alisema wao kama Simba hawana tatizo lolote na wanashukuru kuona
mwekezaji wao Mo amerekebisha kauli ya kujiuzulu na sasa wanaendelea
kumtambua kama Mwenyekiti wao.
“Hilo
limekwisha wanachama watulie, lililotokea jana limefafanuliwa, na
ilikua bahati mbaya, kikubwa kwa sasa tuangalie mbele kwa maendeleo ya
klabu yetu” alisema Magori.
Aidha
Magori amesema wanakabiliwa na kazi kubwa mbele yao hivyo ni vyema
wakawa wamoja na kushirikiana kuunga mkono wachezaji wao katika kipindi
hiki cha kutetea ubingwa wao.
Simba
inatarajia kurejea katika michezo ya Ligi Kuu ikikipiga dhidi ya Mbao,
huku ikiwa bado ipo kileleni baada ya kucheza mechi 14, ikishinda 11 na
kupoteza mmoja na kutoka sare miwili, huku ikiwa na pointi 35 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment