Hivi
karibuni kumekuwa na msemo ambao umeibuka kuwa katika hii dunia muogope
sana Mungu na Teknolojia na pengine kauli hii ya kocha mpya wa
Barcelona, Quique Setien inatudhihirishia hilo baada ya mwaka jana 2019
kabla hata haijajulikana kuwa atakuja kuwa mwalimu wa Muargentina huyo
akisema siku ambayo Messi atatundika daluga kunako soka basi atalia
milele.
Kauli hii iliyoishi mpaka sasa imeibuka upya kwenye mitandao na kupewa uzito mkubwa hasa baada ya yeye kutangazwa rasmi kuwa kocha wa Barcelona ambayo Messi yupo chini yake kwa sasa akiwa kama mwalimu.
Siku zote, Quique Setien amekuwa akivutiwa na soka la Messi hata kabla hajajua kuwa siku moja atakuja kubeba mikoba ndani ya Barcelona.

“Siku
ambayo Messi atatundika daluga, nitalia milele. Hakuna mtu mwingine
kama Messi , nilishapata bahati ya kuona wachezaji wengi wazuri lakini
hawakuwa na muendelezo mzuri na kudumu kwa miaka 12 au 14 ndani ya ubora
ule ule.”
“Naamini
hakuna mchezaji na sifahamu kama Pele katika muda wake alidumu kwenye
ubora wake kwa muda mrfefu kama Messi ndani ya miaka 12.”
“Sifahamu
zaidi idadi ya ‘hat-trick’ ambazo amefunga. Ni furaha kumuona
akijumuishwa kikosini na kumuangalia kila siku ya Jumapili ndani ya
miaka yake hii 12 ama 14.
“Kitu ambacho nakipenda kwa Messi ni kwamba siku zote amekuwa bora na amezidi kudhihirisha hilo kila wikiend.”
Maneno
hayo ya kocha Quique Setien aliyasema baada ya Barcelona kuibuka na
ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Betis huku Messi akitupia mabao matatu
kwenye mechi hiyo mwaka 2019.
Quique Setien alitangazwa kuwa kocha
mpya wa Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili na nusu akichukua mikoba
ya Ernesto Valverde aliyetimuliwa kazi mapema wiki hii.
0 comments:
Post a Comment