IMERIPOTIWA kuwa nyota wa kikosi cha Arsenal, Alexandre Lacazette anaweza kuondoka msimu ujao ndani ya timu hiyo inayonolewa na Mikel Arteta.
Inatajwa kuwa Juventus na AC Milan zipo kwenye hesabu za kuipata saini ya mshambuliaji huyo ambaye Arteta amemuacha afanye maamuzi kuhusu kuondoka ama kubaki.
Atletico Madrid nao pia wanatajwa kusaka saini ya nyota huyo huku wakiwa na matumaini makubwa ya kupata saini yake kwa kuwa watabadilishana na kiungo wao Thomas Partey ambaye anahitajika ndani ya kikosi cha Arsenal.
Arsenal ipo kwenye mchakato wa kusaka saini ya Partey mwenye miaka 27 hivyo nafasi ya kuipata saini yake itaongezeka iwapo watakubali kufanya mabadilishano na mchezaji huyo.
Arteta amesema:"Tunapaswa kuwa na mtazamo kwa ajili ya wakati ujao ila namna ambavyo kila mchezaji anafikiria hiyo inakuwa juu yake, ninafurahi kuwa na Laccazette kwa kuwa anafanya kazi vizuri ila kama atahitaji kuondoka ni mtazamo wake yeye hivyo tusubiri na tuone."
0 comments:
Post a Comment