KlABU ya Chelsea imefungua ukurasa mpya wa mazungumzo na kiungo wao Willian Da Silva raia wa Brazil.
Hatua hiyo imefikia baada ya nyota huyo kugomea ofa ya timu moja kutoka nchini China.
Nyota huyo mwenye miaka 31 amesema kuwa yupo tayari kusaini kandarasi ya miaka mitatu ndani ya Chelsea ila mabosi wake hawapo tayari kumpa miaka hiyo.
Kwa sasa hesabu ni kumshawishi akubali dili la miaka miwili ili abaki ndani ya Stamford Bridge.
Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard inajua kuwa ikimuacha asepe basi anaweza kuibukia Arsenal ama Tottenham Hotspur.
Kibindoni ana mabao 10 ndani ya Ligi Kuu England msimu huu wa 2019/20.
0 comments:
Post a Comment