RASMI nyota wa KMC, Charlse Ilanfya ni mali ya Simba baada ya uongozi wa KMC kuthibitisha jambo hilo.
Ilanfya ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa na KMC ametupia jumla ya mabao sita jambo lililowavutia Simba kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kina taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 na kitaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.
Ilanfya aliibukia ndani ya KMC akitokea Klabu ya Mwadui FC amekuwa kwenye msimu mzuri kwenye mechi za mwisho za KMC kwa kuwa awali alikuwa akisumbuliwa na mejeraha ya misuli ya nyama za paja.
Meneja wa KMC, Walter Harrison amesema kuwa ni Simba pekee walipeleka ofa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo hivyo kwa sasa ni mali ya Simba.
Ilanfya amesema kuwa atapambana kuweza kuwa bora ndani ya maisha yake mapya.
0 comments:
Post a Comment