Wednesday, August 5, 2020



ASTON Villa inaripotiwa imepanga kumuongezea dili jipya nahodha wa kikosi hicho Jack Grealish pamoja na mkwanja wa kumpa nyota huyo.
Lengo la kufanya hivyo ni kumzuia nahodha huyo anayecheza timu moja na Mbwana Samatta raia wa Tanzania kutoibukia ndani ya Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 24 alifunga bao muhimu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England mbele ya West Ham United kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Grealish ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu wa Villa, Dean Smith ambaye amefanikiwa kujinusuru kubaki ndani ya Ligi Kuu England. 
Mkwanja ambao Villa wanapanga kumlipa kwa wiki ni pauni 70,000 na wana matumaini kwamba atabaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

0 comments:

Post a Comment