Wednesday, August 5, 2020



IMERIPOTIWA kuwa, Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anampigia hesabu beki wa Klabu ya  Norwich, Jamal Lewis kwa msimu ujao.
Klopp anahitaji kumuongezea nguvu beki wake, Andy Robertson ambaye alijiunga na kikosi hicho mwaka 2017 akitokea Klabu ya Hull City katika sehemu ya ulinzi ili kuongeza upana wa kikosi chake ndani ya Ligi Kuu England. 
Liverpool ni mabingwa wa Ligi Kuu England wanachokifanya kwa sasa ni kuzidi kuimarisha kikosi hicho ili kiweze kutetea taji hilo.
Nyota huyo mwenye miaka 22, amecheza jumla ya mechi 92 tangu mwaka 2016 na ametupia bao moja kibindoni inatajwa kuwa Liverpool imeweka dau la pauni milioni 10 ili kupata saini yake.
Ikiwa dili hilo litakamilika, Klopp atakuwa na uhakika wa kufanya kazi na nyota huyo ambaye anakubali uwezo wake ndani ya uwanja licha ya timu yake kushuka daraja

0 comments:

Post a Comment