Thursday, November 19, 2020

 

Mchezaji bora duniani Lionel Messi amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa amechoshwa na zigo la lawama analotupiwa ndani ya Barcelona.

messi

Messi amesema kuwa amekuwa akipewa lawama kwa kila matatizo yanayotokea Barcelona, kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa wakala wa Antoine Griezmann, Eric Olhats kudai Mfaransa huyo amekuwa katika wakati mgumu ndani ya klabu kwa sababu ya Lionel Messi.

Eric Olhats amemtuhumu Messi kwa kuwa mtu mwenye udhibiti mkubwa ndani ya Barcelona, akitumia maneno “reign of terror” na kumfanya Griezmann kuwa kwenye wakati mgumu wa ‘ku-adapt tangu alivyotua ndani ya timu hiyo mwaka uliyopita.

Akiwa njiani kurudi Barcelona baada ya majukumu ya kitaifa, Messi alikutana na waandishi wa habari airport ndipo akatoa kauli hiyo “Ukweli ni kwamba kidogo nimechoka kila wakati mimi kuwa matatizo ya kila kitu ndani ya klabu.”

Lionel Messi amewaambia waandishi kuwa ”Juu ya yote hayo, baada ya kusafiri kwa saa 15 angani, mamlaka ya ushuru ilikuwa ikinisubiri, ni wazimu.

Akiwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Barcelona, Messi aliwahi kujaribu kufuatilia kifungu kinachombana yeye kushindwa kuondoka Barcelona kama mchezaji huru na kuamua kusalia ili kukwepa vita dhidi yake na klabu.

Barcelona napitia kipindi kigumu cha machafuko tangu Bayern Munich ilipoidhalilisha timu hiyo kwa kuipa kipigo cha haibu cha goli 8-2 katika michuano ya Champions League hatua ya robo fainali msimu uliyopita kabla hata ya kujiuzuru kwa aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu mwezi uliyopita.

Messi amekuwa na matatizo na mamla ya ushuru nchini Uhispania katika miaka ya hivi karibuni. Aliwahi kupewa kifungo cha miezi 21 gerezani mnamo 2016 na kuamriwa kulipa faini ya paundi milioni 2 baada ya kupatikana na hatia ya kulaghai serikali ya Uhispania ya paundi milioni 4.2 juu ya mapato yaliyopatikana kutoka kwa haki za picha.

0 comments:

Post a Comment