Liverpool na Manchester United wameongeza kasi mbio za kuwania saini ya mchezaji wa RB Leipzig Dayot Upamecano huku Bayern Munich ikiashiria kuwa haina uwezo wa kumsaini nyota huyo mwenye umri wa miaka 22. (Bild, via Mirror)
Manchester United hawana nafasi ya kusaini mkataba na kiungo wa kati- Mfaransa Raphael Varane, 27, kutoka Real Madrid. (Manchester Evening News)
Real Madrid wanakabiliana na Barcelona katika kinyang’anyiro cha kumsaini kiungo wa kati Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, kutoka Liverpool. (Corriere Dello Sport via Sport)
Mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28 ndiye mchezaji anayelengwa zaidi na Real Madrid kama kiungo wa kati-nyuma wa Uhispania Sergio Ramos ataondoka katika klabu hiyo msimu huu . (AS)
0 comments:
Post a Comment