Wednesday, September 29, 2021


 


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu leo Septemba 29 mbele ya Yanga.

Kagera Sugar ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba.

Baraza amesema kuwa anatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu ila watapambana kupata pointi tatu muhimu.

"Ni mchezo mgumu na ushindani mkubwa kwa kila timu lakini kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu.

"Wachezaji wapo tayari na wanajua kwamba mchezo hautakuwa mgumu, mashabiki wajitokeze kuwa nasi bega kwa bega kwani mchezo wa mwanzo unahitaji kushinda ili kujenga hali ya kujiamini," amesema.

Msimu wa 2020/21 walipokutana Uwanja wa Kaitaba, ubao ulisoma Kagera Sugar 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Tonombe Mukoko ambaye leo ataukosa mchezo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho mbele ya Simba

0 comments:

Post a Comment