BREAKING:MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ameamua kukaa pembeni kwenye nafasi hiyo kutokana na makubaliano ya Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba.
Taarifa ambayo ameituma Mo amesema kuwa:"Miaka minne tumepata mafanikio makubwa,tumeshinda ligi mara nne kufanya vizuri Champion League,(Ligi ya Mabingwa Afrika).
"Bado ninaipenda Simba. Tumefanya mkutano wa bodi tarehe 21,9,2021 tumekubaliana kwamba mimi nitastep down, (kuwa pembeni) kuwa chairman (mwenyekiti) Simba SC.
"Ninaomba wanachama wa Simba msifikirie mimi ninaondoka kwenye Simba, mimi bado ni mwanahisa, ninaipenda Simba, tumekubaliana kufanya hivyo kwa sababu mimi nimekuwa ninasafiri sana," .
0 comments:
Post a Comment