Thursday, September 30, 2021

 


WENYEJI, Bayern Munich wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Dynamo Kyiv katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani.
Mabao ya Bayern Munich jana yalifungwa na Robert Lewandowski mawili, dakika ya 12 na 27 akimalizia pasi ya Thomas Müller, Serge Gnabry dakika ya 68, Leroy Sané dakika ya 74 na Erick Choupo-Moting dakika ya 87.
Ushindi huo unawafanya Bayern Munich waendelee kuongoza Kundi E wakifikisha pointi sita, mbele ya Benfica wenye pointi nne, Dinamo Kiev pointi moja na Barcelona ambayo haina pointi.

0 comments:

Post a Comment