KUTOKANA na mwendo ambao wanakwenda nao kwa sasa Manchester United wameambiwa kwamba hawana ubavu wa kutwaa taji la Ligi Kuu England kwa msimu huu ambalo lipo mikononi mwa Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola.
Gary Neville gwiji wa Manchester United ameweka wazi kwamba matumaini kwa timu hiyo kuweza kutwaa taji hilo kubwa kwa sasa ni madogo hasa ukiilinganisha na wapinzani wao kwa kuwa wanacheza bila kushirikiana.
Pia wengine wameshauri kwamba kwa sasa ni muhimu kwa Manchester United kumuweka kando kocha wao Ole Gunnar Solkajaer na kumpa mikoba Antonio Conte kwa kuwa wengi hawamuelewi kocha huyo jambo analolitafuta ndani ya ligi.
Haya yote yamekuja kutokana na mwendo wa kinyonga wa Manchester United kwenye kusaka matokeo ambapo ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Young Boys, ikanyooshwa na West Ham United na Aston Villa kote iliambulia bao mojamoja ilikuwa ni kwenye mechi za Ligi Kuu England.
Kesho Septemba 29 ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Villarreal katika mchezo wa UEFA Champions na haipewi nafasi ya kushinda kutokana na kushindwa kutabirika licha ya uwepo wa nyota mkubwa Cristiano Ronaldo ndani ya kikosi hicho.
"Nafikiri hivi hata pale wanaposhinda na hata Ronaldo anapofunga bado wamekuwa hawachezi vizuri kama timu kwa kushirikiana. Nafikiri wanatakiwa kuungana na kushirikiana," amesema Neville.
0 comments:
Post a Comment