TIMU ya Liverpool imelazimisha sare ya 3-3 na wenyeji, Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Brentford Community mjini Brentford, Middlesex.
Mabao ya Brentford yamefungwa na Ethan Pinnock dakika ya 27, Vitaly Janelt dakika ya 63 na Yoane Wissa dakika ya 82, wakati ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 31, Mohamed Salah dakika ya 54 na Curtis Jones dakika ya 67.
Liverpool inafikisha pointi 14 baada ya mchezo huo na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani pointi moja tu zaidi ya Manchester City, Chelsea na Manchester United baada ya wote kucheza mechi sita.
Liverpool inafikisha pointi 14 baada ya mchezo huo na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani pointi moja tu zaidi ya Manchester City, Chelsea na Manchester United baada ya wote kucheza mechi sita.
0 comments:
Post a Comment