Wednesday, September 29, 2021



MABAO ya Idrissa Gueye dakika ya nane na Lionel Messi dakika ya 74 jana yamewapa wenyeji, Paris Saint-Germain ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa.
Ushindi huo unaipeleka kileleni mwa Kundi hilo PSG ikifikisha pointi nne baada ya mechi mbili, sawa na Club Brugge, wakati Manchester City inabaki na pointi zake tatu katika nafasi ya tatu, mbele ya RB Leipzig ambayo haina pointi baada ya mechi mbili za awali.

0 comments:

Post a Comment