Tuesday, September 28, 2021

 


TIMU ya Namungo FC imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Namungo FC, timu kutoka Ruangwa yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 13 na Relliant Lusajo dakika ya 81.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wageni wakitangulia kwa bao la beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 49, kabla ya Hance Masoud kuwasawazishia wenyeji dakika ya 90.
Na wageni wengine, Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao pekee la William Edgar dakika ya 50 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

0 comments:

Post a Comment