Thursday, September 30, 2021

 


CEDRIC Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa nguvu kwa timu hiyo zinaelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,  Oktoba 2.


Jana Septemba 29, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na mtupiaji wa bao alikuwa ni Feisal Salum aliyemtungua kipa wa Kagera Sugar,  Chalamanda.


Kaze amesema wataendelea kukijenga kikosi na timu itazidi kuimarika sasa wakielekeza nguvu zao katika mchezo unaofuata


"Mechi ya kwanza ya ligi, ushindi ugenini, tunaendelea kujenga timu na tutaimarika zaidi. Mechi inayofuata inakuja  siku 3 mbele, dhidi ya Geita Gold, tuko nyumbani,".


Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.


Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije mchezo wake wa kwanz ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Namungo.

0 comments:

Post a Comment