Friday, October 15, 2021

 



BODI ya Ligi ya Tanzania (TPLB) imesogeza mbele mechi ya Ligi Kuu baina  ya mabingwa watetezi, Simba SC na Polisi Tanzania uliokuwa ufanyike Oktoba 20 hadi Oktoba 27.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema hatua hiyo imefuatia barua ya Simba SC wakiomba mechi hiyo isogezwe kwa sababu wamekosa ndege ya kuwahi kurejea nchini baada ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Jwaneng Galaxy FC Jijini Gaborone nchini Botswana Jumapili.


0 comments:

Post a Comment