Friday, October 15, 2021

 



ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Mzambia Clatous Chota Chama ambaye kwa sasa anachezea RS Berkane ya Morocco atawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita.
Chama atawania tuzo hiyo dhidi ya nyota wa Yanga, viungo pia Mkongo Tonombe Mukoko na Mzanzibari, Feisal Salum ' Fei Toto' katika hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.







0 comments:

Post a Comment