KITENDO cha mabosi wa Yanga kushindwa kujibu tuhuma za kuwafanyia vurugu wapinzani wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Rivers United inaelezwa kuwa kimewagahrimu faini ya milioni 11.
Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) limeipiga faini hiyo Yanga kwa kushinda kujibu tuhuma za kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.
Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United.
Rivers waliweza kuripoti Caf na kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu wao ikiwa ni pamoja na Ofisa Habari wa timu hiyo, Charles Mayuku.
CAF imesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani jambo ambalo limesababisha pia Yanga kupigwa faini.
CAF imesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani jambo ambalo limesababisha pia Yanga kupigwa faini.
Habari kutoka Yanga imeeleza kuwa kwa sasa ishu hiyo bado haijawa rasmi zaidi ya kuwa tetesi.
0 comments:
Post a Comment