Friday, October 15, 2021

 


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtza Mangungu amesema sababu iliyopelekea kushindwa kusafiri na ndege walioingia nayo mkataba kupitia ATCL ni kutokana na sababu nyingi ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao licha ya kufanya maandalizi mazuri kwa wakati.

Mangungu ameyasema hayo kupitia kipindi cha Michezo cha ‘Kipenga’ cha East Africa Radio kilichoruka jana Oktoba 13, 2021 kuanzia saa 2:00 hadi 3:00 usiku aambapo alihojiwa kwanini hawajasafiri na ndege ambayo Septemba 17, 2021 waliingia nayo mkataba wa miaka miwili kuwaweza kusafiri ndani nan je ya mipaka ya Tanzania.

Mangungu amejibia kwa kusema, "Tuna mikataba sio na ATCL pekeake, tuna mikataba na taaasisi nyengine nyingi na tunatumia facilities hizo pale ambapo kuna uwezekano wa kutumia kulingana na ratiba ya hao tulioingia nao mikataba na kadharika".

"Tumejiandaa vizuri na tutakwenda kwasababu ninayokueleza, Hiyo Botswana kwanza ni mara ya kwanza Simba inaenda kucheza huko, na siamini kwamba tumeshindwa kufanya taratibu kama inavyotakikana”.

“Tumefanya taratibu lakini kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa yafanyike, Hata hao nyinyi mnaowatamka (ATCL) tuliofanya nao mkataba, ili ndege iende kutua kule zipo taratibu za kiusalama ambazo zinatakiwa zifanyike”.

“kabla hazijakuwa confirmed hatuwezi kuhakiki kusema kwamba tutasafiri na ndege fulani saa fulani muda fulani"

Mwisho akamaliza kwa kutupa kijembe kwa wanaoiombea mabaya Simba kuwa wajiandae kukaa mkao wa kula kwani Simba itaendelea kufanya vizuri.

"Wale wanaoitakia mema Simba waendelee kuitakia mema Simba, na wale wanaoitakia mabaya waendelee kusubiria wakiiona Simba  ikiendelea kufanya vizuri". Amesema Mangungu.

Simba inataraji kuondoka nchini Ijumaa ya kesho Oktoba 15, 2021 kuelekea nchini Botswana ambapo itakuwa na mchezo wa kwanza wa second preliminary round kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwanenga Galaxy kabla ya kurudiana nao Oktoba 24, 2021 kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

 

0 comments:

Post a Comment