Friday, December 31, 2021

 


WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya nane, Ben Mee aliyejifunga dakika ya 27 katika harakati za kuokoa krosi ya Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo aliyekamilishwa shangwe za ushindi dakika ya 35.
Kwa ushindi huo, Manchester United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya sita, wakati Burnley inabaki na pointi zake 11 za mechi 16 sasa katika nafasi ya 18.

0 comments:

Post a Comment