Tuesday, January 18, 2022


Karim Benzema ametishia kuondoka Real Madrid msimu ujao kama Klabu hiyo itamsajili, Erling Haaland kwa mujibu wa ripoti, huku mshambuliaji huyo ikisemekana kukosa furaha mbele ya Florentino Perez.

Benzema mwenye umri wa miaka 34, aameshafunga jumla ya magoli 24 kwenye michezo yake 27 aliyocheza msimu huu lakini Real Madrid ipo kwenye mstari wa mbele kwenye mbio za kumsajili, Haaland endapo atatimka Borussia Dortmund kipindi cha majira ya joto.

Kwa hali hiyo, Florentino Perez atapaswa kuchagua moja kubaki na Benzema ama kumsajili Erling Haaland. Benzema amemwambia pia, Perez kwamba yupo radhi kuendelea kubakia Madrid kama hatosajiliwa Mnorway huyu.

0 comments:

Post a Comment