TIMU ya Mbeya City imeendeleza wimbi la ushindi nyumbani katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Bao pekee la ‘Wana Koma Kumwanya’ leo limefungwa na Aziz Andambwile dakika ya 54 na kwa ushindi huo MCC wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya tatu, wakizidiwa pointi mbili tu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
Ruvu Shooing kwa upande wao baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 pia katika nafasi ya 14.
0 comments:
Post a Comment