Friday, January 21, 2022

 


Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Real Madrid inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe ,23, kutoka PSG , na atajiunga kama mchezaji huru wakati kandarasi yake itakapokamilika. (ESPN)

Paris St-Germain iko katika mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, kwa mkopo . Ndiye mchezaji aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa wakati akijiunga na klabu hiyo 2019 kwa dau la £53m. (Goal)

Sevilla bado inataka kumsaini mshambuliaji wa Man United na Ufaransa Anthony Martial , 26, kwa mkopo licha ya ombi lao kukataliwa , inaweza pia kumtafuta mshambuliaji mwengine wa Ufaransa - Moussa Dembele, 25 wa Lyon - kama mbadala wake. (Marca)

Anthony Martial

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester United itamruhusui winga wa England Jesse Lingard, 29, kuondoka kabisa mwezi huu, huku Newcastle ikiwa na hamu ya kumsaini. Hatahivyo , Red Devils hawatamruhusu Lingard kujiunga na West Ham au Tottenham kwa kuwa hawataki kuimarisha wapinzani wao waliopo katika nafasi nne bora katika jedwali la ligi ya Premia. (Sky Sports)

Newcastle United wamewasilisha ombi la dau la £14.5m kumnunua beki wa kushoto wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Mitchel Bakker, 21. (Mail)

Tottenham inafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast franck Kessie, 25 wakati wa dirisha la uhamisho. (Telegraph, subscription required)

paul Pogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba hajaiambia Manchester United iwapo anataka kusalia katika klabu hiyo zaidi ya mwisho wa msimu huu wakati kandarasi yake itakapokamilika . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anatakiwa na PSG , Real Madrid na Juventus. (90 min)

Timu mbili , ikiwemo moja nchini Ujerumani , zina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele kwa mkopo baada ya mchezaji huyo mweye umri wa miaka 24 aliyejiunga na Barcelona kwa dau la £135m 2017, kuambiwa kuondoka kwasababu hataki kutia Saini kandarasi mpya. (Sport)

Beki wa Itali mshindi wa kombe la Dunia Fabio Cannavaro, 48, amehojiwa na Everton kuhusu wadhfa wa ukufunzi ulio wazi katika timu hiyo . Cannavaro alikuwa akisimamia kikosi cha China cha Guangzhou Evergrande hadi mwezi Septemba. (Telegraph, subscription required)

Fabio Canavarro

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mkufunzi wa Watford Claudio Ranieri amethibitsha kwamba klabu hiyo ipo katika harakati za kumsaini winga wa Bordeaux na Nigeria Samujel Kalu kwa dau la £3m, na pia ina hamu ya kumsajili beki wa Liverpool Nathaniel Phillips, 24. (Evening Standard)

0 comments:

Post a Comment