Novak Djokovic ameondoka Australia baada ya kushindwa kukubaliwa ombi lake la mwisho katika mahakama la kutaka kubaki nchini humo.
Majaji walikataa changamoto iliyoletwa na nyota huyo wa tenisi ambaye hakuwa amechanjwa baada ya serikali kufuta visa yake kwa misingi ya "afya na utaratibu mzuri".
Matumaini ya mchezaji huyo nyota duniani za kutetea taji lake la wazi la Australian Open na kushinda rekodi ya 21 ya Grand Slam mjini Melbourne yamekamilika.
Djokovic alisema "amesikitishwa sana" lakini alikubali uamuzi huo.
Alipanda ndege iliyokuwa ikielekea Dubai kutoka uwanja wa ndege wa Melbourne.
Alipokuwa akijiandaa kuondoka, bodi inayosimamia tenisi ya wanaume ATP ilisema uamuzi wa mahakama siku ya Jumapili iliashiria mwisho wa "msururu wa matukio ya kusikitisha sana".
Mapema siku hiyo, wafuasi wa Djokovic walikaa kimya nje ya chumba cha mahakama huku uamuzi huo ukitangazwa usiku wa kuamkia mechi yake ya ufunguzi katika dimba hilo.
Shabiki mmoja aliiambia BBC kwamba majira yake ya joto yatakuwa "tupu" bila mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kucheza kwenye Open.
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison alikaribisha "uamuzi wa kuweka mipaka yetu imara na kuwaweka Waaustralia salama".
Djokovic alianzisha kesi hiyo baada ya Waziri wa Uhamiaji Alex Hawke kutumia mamlaka yake ya uwaziri kufuta viza ya mchezaji huyo wa Serbia, akihoji kuwa uwepo wake nchini humo unaweza kuhatarisha hisia za kupinga chanjo.
Ilikuwa ni mara ya pili kwa visa yake kufutwa, baada ya kughairiwa kwa mara ya kwanza kwa kutofuata sheria za marufuku dhidi ya Covid kubatilishwa na jaji tofauti.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakamani siku ya Jumapili mbele ya jopo la majaji watatu, upande wa utetezi wa Djokovic ulidai bila mafanikio kwamba sababu zilizotolewa na serikali "zilikuwa batili na zisizo na mantiki".
Jaji Mkuu James Allsop alisema uamuzi wa mahakama ya shirikisho uliegemea juu ya uhalali wa uamuzi wa waziri, na sio kuwa ulikuwa uamuzi sahihi.
Sababu kamili za uamuzi huo zitawekwa wazi katika siku zijazo, alisema.
Maagizo hayo yalijumuisha marufuku ya miaka mitatu ya kutoingia Australia, ingawa hii inaweza kuangaziwa katika mtazamo tofauti.
Kumekuwa na hasira nyingi kutoka kwa umma nchini Australia kuhusu jaribio la mchezaji huyo kuingia nchini humo bila ya kupata chanjo dhidi ya Covid-19.
Serikali ya shirikisho lilisema kuwa mara kwa mara watu lazima wazingatie sheria zilizowekwa za kukabiliana na janga hili, na kwamba hakuna mtu yuko "juu ya sheria".
Awali Djokovic alipewa msamaha wa matibabu kuingia Australia na makundi mawili tofauti ya watalaamu wa afya - moja iliyoidhinishwa na tume ya Tennis Australia, nyingine na serikali ya jimbo la Victoria - baada ya kupimwa kuwa na ugonjwa wa coronavirus katikati ya Disemba.
Hata hivyo kikosi cha mpakani cha Australia kilimzuia mnamo Januari 5 kwa kutokidhi mahitaji ya serikali ya coronavirus, na visa yake ikafutwa.
Baadaye jaji alibatilisha uamuzi huo, lakini serikali iliingilia kati Ijumaa iliyopita ili kufuta visa tena, ikisema kufanya hivyo ni kwa manufaa ya umma.
Ingawa Djokovic hajachanjwa dhidi ya Covid-19, hajahimiza kikamilifu habari za kuzuia chanjo. Hata hivyo, wapinga vaxxers wa Australia wamekuwa wakitumia kampeni ya #IStandWithDjokovic kwenye mitandao ya kijamii.
Mapambano ya kupata visa pia ni kitovu cha mzozo wa kisiasa nchini humo.
Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Bw Morrison alisema serikali "imejiandaa kuchukua maamuzi na hatua zinazohitajika ili kulinda uadilifu wa mipaka yetu".
Lakini mwanasiasa wa upinzani nchini Australia Kristina Keneally alisema Bw Morrison alijifanya kuwa "mcheshi" kwa kushughulikia vibaya kesi ya Djokovic, huku akihoji ni kwa nini mchezaji huyo ambaye hakuwa amechanjwa alipewa visa mara ya kwanza.
Bw Morrison na serikali yake pia walikabiliwa na hasira kutoka kwa Rais wa Serbia Aleksandar Vucic.
"Yeye [Djokovic] alikuja Australia na pendekezo la msamaha wa matibabu na kisha ukamtesa kwa siku 10. Kwa nini ulifanya hivyo? Kufanya uwindaji wa wachawi dhidi yake? Hili ni jambo ambalo hakuna mtu anayeweza kuelewa," alisema.
Shirikisho la tenisi la wanaume ATP liliita sakata hiyo "msururu wa matukio ya kusikitisha sana", huku nyota wa tenisi wa Uingereza Andy Murray akisema hali si nzuri kwa yeyote.
Djokovic, siku ya Jumapili alisema "hakuwa na raha" kutokana na kuangaziwa yeye na mzozo wake wa visa, na kuongeza: "Ninatumani kwamba sote sasa tunaweza kuzingatia mchezo na mashindano ninayopenda."
Australian Open angeweza kumfanya Djokovic kuweka historia kwa kushinda Grand Slam yake ya 21.
Salvatore Caruso wa Italia, aliyeorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani, ndiye "mshindi mwenye bahati" ambaye sasa atachukua nafasi ya Djokovic katika mechi yake dhidi ya Miomir Kecmanovic wa Serbia siku ya Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment