WENYEJI, Liverpool wamefufua matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa at Anfield.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 44, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 69 na Takumi Minamino dakika ya 77 na kwa ushindi huo kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 45 katika mchezo wa 21, kikizidiwa pointi 11 na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Brentford yenyewe inabaki na pointi zake 23 za mechi 21 katika nafasi ya 14.
0 comments:
Post a Comment