Thursday, January 20, 2022

 


Robert Lewandowski

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski

Bayern Munich wanaweza kuamua kumuuza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski msimu wa joto ikiwa hatatia saini mkataba mpya uliorefushwa, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ukitarajiwa kukamilika mwezi Juni 2023. (Bild, via Marca)

Wawakilishi wa Cristiano Ronaldo wameiambia Manchester United kwamba mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 anapania kuondoka Old Trafford msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Sun)

Atletico Madrid haitamruhusu mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 34, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Aston Villa, kuondoka mwezi Januari. (Goal)

Suarez scores

CHANZO CHA PICHA,NURPHOTO

Maelezo ya picha,

Atletico Madrid haitamruhusu mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 34 kuondoka

Barcelona wamepiga hatua katika mazungumzo kumhusu mlinzi wa Chelsea Andreas Christensen, 25, huku kandarasi ya mchezaji huyo wa Denmark ikitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sport - kwa Kihispania)

Manchester United itamruhusu kiungo mshambuliaji Jesse Lingard kuondoka mwezi Januari ikiwa klabu italipa ada ya mkopo ya £3.5m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye kandarasi yake huko Old Trafford inakamilika msimu wa joto. (Talksport)

Rais wa Lille Olivier Letang anasema klabu hiyo ya Ufaransa "haitafungua hata mlango wa kujadili" kumuuza mlinzi wa Uholanzi Sven Botman, huku Newcastle United na AC Milan zikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Football Italia)

Jesse Lingard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Jesse Lingard.

Arsenal wameongeza kasi ya kumsaka kiungo wa Juventus Arthur Melo, huku The Gunners wakitumai kumsajili Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Goal)

Arsenal pia wako tayari kumfanya fowadi wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, mmoja wa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia hajaamua ikiwa anataka kuhamia The Gunners. (La Nazione via 90Min)

Juventus wamechukizwa na kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kukataa ofa ya kuwahama Waitaliano hao kutoka vilabu vya Uingereza na Uhispania.(Calciomercato, kupitia Mail)

Aaron Ramsey

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Juventus wamechukizwa na kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey

Bayern Munich wako tayari kukabiliana na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uswizi na Borussia Monchengladbach Denis Zakaria, 25.(Christian Falk)

Paris St-Germain wana uhakika kwamba kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 49, ataiongoza Parc des Princes msimu ujao. (Marca)

AC Milan wanataka kumsajili kwa mkopo beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 22- Japhet Tanganga, lakini klabu hiyo ya Ligi ya Primia ingependa kumuuza kiungo huyo Muingereza. (Sun)

Japhet Tanganga wa Spurs (kulia) akichuana na Sadio Mane wa Liverpool

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Japhet Tanganga wa Spurs (kulia) akikabana na Sadio Mane wa Liverpool

Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa na Arsenal Thierry Henry yuko katika kinyang'anyiro cha kuwa kocha wa Bordeaux atakapojiondoa kama mkufunzi wa Montreal Impact mwezi Februari. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Stoke wanajiandaa kumsaini winga wa Aston Villa wa miaka 19- Muingereza Jaden Philogene-Bidace kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Athletic - usajili unahitajika)

0 comments:

Post a Comment