Monday, January 8, 2018


Rafiki yangu mmoja ni shabiki mkubwa sana wa Lioneil Messi na siku moja aliwahi kuniambia “Messi hanuniwi, ukimnunia utakonda”, msemo huu nimeukumbuka leo baada ya kumuona Messi akifunga zidi ya Levante.
Bao hili limemfanya Lioneil Messi kuandika rekodi mpya ya mabao 365, ni Gerrad Muller pekee ambaye amewahi kufunga mabao 365 katika ligi moja barani Ulaya na sasa Messi anakuwa amemfikia Muller.
Hii ina maana kama Lioneil Messi atafunga bao moja tu katika michezo aliyobakisha kucheza baasi nyota huyu wa Kiargentina atakuwa mchezaji wa kwanza barani Ulaya kufunga mabao 366 katika ligi moja.
Lakini wakati Messi akiifikia rekodi ya Gerrard Muller, hii leo pia mchezaji huyo alifikisha jumla ya michezo 400 akiwa na klabu ya Barcelona, katika michezo hiyo 400 Messi amefanikiwa kufunga mabao 365 na kutoa assist 142 akibeba makombe 30.
Wakati Lioneil Messi akifanya hayo, pacha wake uwanjani ambaye ni Luis Suarez naye amefanikiwa kufikisha mabao 132 akiwa na La Liga na sasa anakaa juu ya Samuel Etoo mwenye mabao 131,.

0 comments:

Post a Comment