Monday, March 5, 2018


Moja kati ya habari kubwa katika michezo iliyochukua headlines kubwa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na kifo cha mchezaji wa zamani wa AC Milan aliyekuwa anaichezea Fiorentina kwa sasa Davide Astori amefariki.

Kifo cha Davide Astori ambaye ni nahodha wa Fiorentina na alikuwa akijiandaa na mchezo wa leo wa Ligi Kuu Italia dhidi ya Udinese kimetokea akiwa amelala hotel walipokuwa wamefikia na timu yake wakisubiri muda wa game dhidi ya Udinese.

Kufuatia kifo cha Davide Astori game zote za Serie A nchini Italia zimeahirishwa lakini kama hufahamu Davide Astori nikukumbushe vitu vitatu kutoka kwake amewahi kuichezea timu ya taifa ya Italia jumla ya game 14, wenzake walienda kuvunja mlango wa chumba chake cha hotel baada ya kutomuona wakati wa chai.

Davideo Astori amefariki akiwa na umri wa miaka 31 na ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka miwili Vittoria, aliyempata kwa mpenzi wake  Francesca Fioretti, taarifa za awali zinaeleza kuwa kifo chake kinatajwa kuwa ni cha kawaida kinachoweza kumkuta binadamu yoyote akiwa usingizini.

0 comments:

Post a Comment