Tuesday, August 14, 2018


MECHI ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Yanga SC iliyopangwa kufanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Agosti 23, mwaka huu imehamishiwa Uwanja wa Uhuru mjini Morogoro katika siku hiyo hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema kwamba wamelazimika kufanya mabadiliko hayo baada ya wamiliki wa Uwanja kusema siku hiyo watakuwa wanautumia kwa shughuli nyingine.
Kwa sababu hiyo, Wambura amesema kwamba Mtibwa Sugar watakwenda kuanzia ugenini dhidi ya Yanga katika mzunguko wa kwanza wa ligi na mchezo wa marudiano utafuatia nyumbani.

Mtibwa Sugar wataanzia ugenini dhidi ya Yanga katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu

Pamoja na hayo, Wambura amesema kwamba mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu za klabu ya Simba SC zilizokuwa zichezwe Uwanja wa Taifa, dhidi ya Tanzania Prisons Agosti 22 na Mbeya City Agosti 25 zitahamishiwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Wambura amesema kwamba hiyo ni baada ya Serikali, wamiliki wa viwanja hivyo kusema Uwanja wa Taifa utakuwa na shughuli nyingine Agosti 22 na 25 na kwamba Simba SC wataruhusiwa kucheza mechi yao ya tatu ya Ligi dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Septemba 1, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment