Tuesday, August 14, 2018


Mchezaji wa Chelsea, Willian Borges da Silva amesema kuwa asingekuwa nasababu ya kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo kama aliyekuwa meneja wao, Antonio Conte angesalia kwenye timu hiyo.

Maneno hayo yanadhihirisha wazi kuwa wawili hao hawapikiki chungu kimoja kwani nikweli kuwa Willian aliamua kuendelea kubaki the Blues mara baada ya Conte kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Maurizio Sarri mapema mwezi Julai.

Alipo ulizwa na juu ya hatma yake ndani ya Chelsea alipokuwa na Conte , Willian amesema asingekuwa na nafasi ya yeye kuendelea kuitumikia timu hiyo na badala yake angefanya maamuzi ya kuondoka.
Nipo hapa kwasababu nahitaji kuichezea Chelsea na ningeondoka kama timu hii ingehitaji mimi nifanye hivyo. Kama Antonio Conte angeendelea kubaki ningeamua kuondoka.
Klabu za Manchester United na Barcelona zote kwapamoja zilionyesha nia yakuhitaji huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwenye dirisha hili la usajili lililopita hii ni kutokana na Willian kutokuwa na mahusiano azuri na Conte.
Willian amefunga jumla ya mabao 44 katika michezo 238 aliyopata kuitumikia Chelsea tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Anzhi Makhachkala  mwaka 2013.

0 comments:

Post a Comment