Tuesday, August 14, 2018



Jina la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri na club ya Liverpool ya England Mohamed Salah limeingia matatizoni baada ya polisi nchini England Liverpool kuanza uchunguzi kuhusiana na video inayodaiwa kusambaa mitandao.

Mohamed Salah imeripotiwa kuwa kuna video imesambaa katika mitandao ya kijamii akionekana akiendesha gari huku akichezea simu, kitu ambacho ni kosa kisheria, taarifa za kosa hilo zinazoendelea na uchunguzi zinadaiwa kuripotiwa Polisi na viongozi wa club ya Liverpool wenyewe.

Video ya Mohamed Salah akichezea simu huku akiendesha gari inadaiwa ilikuwa ni siku ya game ya Liverpool dhidi ya West Ham United iliyomalizika kwa Liverpool kupata ushindi wa magoli 4-0, kama Mohamed Salah itathibitika katenda kosa hilo atakutana na adhabu.

Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”

0 comments:

Post a Comment