Friday, September 7, 2018


Gareth Bale akishangilia baada ya kuifungia Wales bao la pili dakika ya 18 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Ireland usiku wa jana Uwanja wa Cardiff City kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa Ulaya, hilo likiwa bao lake la 30 anaifungia timu yake hiyo ya taifa katika mechi ya 71 kucheza. Mabao mengine ya Wales yalifungwa na Tom Lawrence dakika ya sita, Aaron Ramsey dakika ya 37 na Connor Roberts dakika ya 55 huku la Ireland likifungwa na Shaun Williams dakika ya 66

0 comments:

Post a Comment