Thursday, January 16, 2020

 MATA AWAONGEZEA KASI MANCHESTER UNITED KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA LIVERPOOL

JUAN Mata aliwaamsha mashabiki wa Manchester United dakika ya 67 kwa kufunga bao pekee la ushindi mbele ya Wolves kwenye mchezo wa FA raundi ya tatu.

Ushindi huo unaifanya Manchester United iliyo chini ya Ole Gunnar Solskjaer kusonga mbele wakisubiri mshindi kati ya Watford ama Tranmere kwenye raundi ijayo.


Ushindi huo uwemewapa nguvu ya kujiamini kuelekea mchezo wake wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool utakaopigwa Jumapili licha ya kuumia kwa mshambuliaji wake Macus Rashford.

United iliyo nafasi ya tano kwenye ligi itamenyana na Liverpool iliyo nafasi ya kwanza na ina pointi 61 baada ya kucheza mechi 21 huku United ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 22.

Mechi ya kwanza iliyopigwa Old Trafford, United ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Liverpool ambao hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment