Thursday, January 16, 2020



Baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kunako Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima, amesema timu haikustahili kubadilisha kocha.

Malima ameeleza kuwa Yanga ilipaswa kuendelea kumwamini na kumtumia Mkwasa sababu tayari alikuwa ameshaanza kuwaweka sawa wachezaji kitimu.

Mchezaji huyo amefunguka akieleza kuwa Mkwasa alikuwa ameshaanza kuwapa somo wachezaji baada ya aliyekuwa kocha Mwinyi Zahera kuwaacha na walianza kuja vizuri lakini ameshangazwa na Yanga kumtoa Mkwasa.

"Unajua Yanga mimi nawashangaa sana kuleta kocha mwingine.

"Mkwasa tayari alikuwa ameshaanza kuwapa somo vijana na walianza kumwelewa, kwanini tena waachane naye na walete kocha mwingine.

"Sijaafiki, kuleta kocha mwingine kunazidi kuirudisha timu nyuma na ni maamuzi ambayo mimi sijayapenda."

0 comments:

Post a Comment