PHILIPPE Coutinho, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Bayern Munich kwa mkopo akitokea Barcelona anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho msimu ujao.
Nyota huyo hajawa kwenye ubora wake mkubwa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Kocha wa Bayern Munich, Hans Dieter Flick amekuwa hampi nafasi ya mara kwa mara nyota huyo hata wakati ule alipokuwa fiti.
Miongoni mwa timu ambazo zinamtazama kwa jicho la karibu ni pamoja na Chelsea, Arsenal na Tottenham Hotspur ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.
Mkataba wake wa mkopo ndani ya Munich unameguka Juni 30 ila bado anapenda kubaki ndani ya kosi hilo.
0 comments:
Post a Comment