Thursday, May 28, 2020

Jadon Sancho celebrates scoring

 Sancho amekuwa akiuguza jeraha ligi ya Ujerumani iliporejelewa, lakini anatarajiwa kucheza mechi ya Jumanne dhidi ya Bayern Munich
Jadon Sancho anachukua mpira upande wake wa kulia ya uwanja na anaanza kutamba nao , akichenga wachezaji kadhaa.
Ana mengi ya kufanya anapofika katika lango la upinzani , lakini hufunga kwa urahisi na kumfanya kipa kuruka upande tofauti.
Mechi hiyo ni ya kirafiki kabla ya msimu wa 2019-20 huku wapinzani wao Seattle Sounders wakiwa wameshindwa katika kila safu ya uwanja kufikia kiwango cha mchezo wa Borusia Dortmund, ni bao ambalo litakufanya kusimama.
Ni mchezaji mwenye kipaji, jasiri na ni mzuri kama vile Lionel Messi.
Sancho amevutia maoni tofauti tangu kufanya uamuzi wake kuondoka Man United ili kutafuta klabu itakayompatia fursa ya kushiriki mechi nchini Ujerumani mwezi Agosti 2017.
Lakini ni jinsi mchezo wake unavyofanana na ule wa mshambuliaji huyo wa Argentina - ufupi wake , uwezo wake wa kutamba na mpira bila wasiwasi na ufungaji wake wa mabao - unavyowavutia mashabiki wa klabu ya Dortmund pamoja na wale wa England.
Baada ya kutoka katika umri wa ujana tarehe 25 mwezi Machi, Sancho sasa anakabiliwa na muongo utakaoamua mchezo wake.
BBC Sport imeangazia takwimu za mchezaji huyo iwapo anaweza kuwa mrithi wa muda mrefu wa Lionel Messi.

Kijana shupavu

Tangu alipokuwa katika klabu ya Man City hadi kufikia katika ligi ya Bundesliga na kupata nafasi ya kuiwakilisha timu ya England - kuimarika kwa Sancho tangu ajiunge na Dortmund kumekuwa kwa kasi.
Sancho Akiwa katika ligi ya Bundesliga
Msimu Mechi alizoshirika Magoli Usaidizi
2017-18 12 1 4
2018-19 34 12 17
2019-20 25 14 17
Magoli 27 ya ligi ya Bundesliga aliyofunga kabla ya kufikisha miaka 20 yanamfanya kuwa mshambuliaji kijana aliyefunga magoli mengi katika historia ya ligi hiyo - ikiwa ni magoli matatu zaidi ya mshambuliaji wa Ujerumani Kai Haverts, ambaye alifikisha miaka 20 mwaka mmoja ulioipita.
Ijapokuwa aliongeza uwezo wake wa kufunga magoli mwaka ulioafuatia , kabla ya kufika umri wa miaka 20 tarehe 24 mwezi Juni 2007, Messi alikuwa amefunga magoli 21 ya la Liga.
Ulinganishi mwengine ni kwamba mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo - mtu wa pekee ambaye anaweza kufikia rekodi ya Messi karne hii alifunga magoli 11 katika ligi hiyo kabla ya kufikia umri wa miaka 20 tarehe 5 Februari 2005.
Ukijumlisha idadi ya magoli ya Sancho na pasi alizotoa na kusababisha magoli kama kijana , sio tu kwamba yuko mbele ya ushindani nchini Ujerumani, yuko mbele ya mshambuliaji yoyote mwenye umri mdogo barani Ulaya.

Magoli yaliofungwa na vijana katika ligi tano kuu Ulaya msimu wa 2018-19

  • Jadon sancho 55
  • Dwight McNeil 15
  • Erling Haaland 12
  • Dejan Kulusevski 12
  • Ferran Torres 11
Kama unavyoweza kuona , kuna pengo kubwa kati ya idadi ya magoli yaliomshirikisha Sancho tangu 2018-19 na mchezaji mwengine anayemfuta Ulaya.
Takwimu hizo za kuvutia dhidi ya mchezaji mwenye umri wowote katika ligi tano kuu Ulaya tangu Agosti 2018 , zinamfanya kuwa katika nafasi ya nne baada ya Roberto Lewandowski , Kylian Mbappe na Messi.

Magoli yaliosababishwa na wachezaji tangu msimu wa 2018-19

  • Lionel Messi 80
  • Kyliam Mbappe 63
  • Roberto Lewandowski 58
  • Jadon Sancho 55
Takwimu pia zinaonyesha wachezaji waliocheza zaidi ya dakika 500 katika ligi tano kuu barani Ulaya.
Anashambulia na kufunga
Kile kinachomweka Sancho mbele ya wenzake akimfukuzia Messi ni weledi wake mbele ya goli.
Kama mashambuliaji anayecheza katika wingi huenda asipate fursa sawa na zile za mshambuliaji aliye katikati, lakini yuko sawa na mshambualiji yeyote anayecheka na wavu mara kwa mara.
Kiwango cha ufungaji wake ni asilimia 30.2 na ni wa pili baada ya mshambuliaji mwenza Paco Lacacer katika ligi tano kuu barani Ulaya katika mismu wa 2018-19.

Kubeba mzigo

ulinganishaji mwengine kati ya Mesi na Sancho ni uwezo wao wa kutamba na mpira kufunga magoli, kipaji ambacho mchezaji huyo wa England alionyesha siku ya Jumamosi baada ya kupata pasi na kutamba na mpira na kumpatia Acraf Hakimi aliyefunga goli la pili dhidi ya Wolfsburg.
Sancho ametoa usaidizi wa magoli 21 ya ligi akiichezea timu yake kupitia ufungaji ama usaidizi wa kutoa pasi itakayosababisha bao katika msimu 2018-19.
Jumla ya magoli aliofunga tangu mwanzo wa msimu wa 2018-19 yanamweka juu akiwa na magoli 21 na Messi pamoja na nyota wa PSG anayepigiwa upatu kumrith gwiji huyo wa Argentina Kylian Mbappe.

0 comments:

Post a Comment